Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezindua mpango mkakati wa kutangaza fursa zilizopo Sekta ya Utalii katika Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga, ili kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuikuza sekta hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es salaam katika Kongamano la Uwekezaji la Swahili International Tourism Expo, wenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko katika wilaya hiyo ikiwemo utalii katika Mbuga ya Saadani, fukwe, Kilimo Biashara pamoja na uchumi wa Buluu.

Amesema, “niwapongeze sana watu wa Pangani kupitia Mkuu wa wilaya kwa ubunifu huu wa hali ya juu na nitoe wito kwa wilaya zingine kuiga Pangani na kufungua fursa za utalii na uwekezaji kwenye wilaya zao.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema sekta ya utalii kwa sasa mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 17 na Serikali itaendelea kuboresha mazingira rafiki katika sekta hiyo ili kuendelea kuvutia utalii nchini katika maeneo mbalimbali hususan wilaya ya Pangani.

Awali, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah alisema, Wilaya ya Pangani imejikita kwenye uwekezaji wa maeneo matatu ikihusisha utalii, Kilimo mkakati na uchumi wa buluu na kuongeza kuwa Wilaya hiyo ni miongoni mwa Wilaya ya kimkakati yenye mazingira mazuri ya uwekezaji.

Tuzo: Malawi yaukubali mchango wa Tanzania
Wakazi Ilembo waikubali Serikali, DC Malisa awapa neno