Neema Mbuja – Kampala.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Oktoba 10, 2023 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda, ili kupeana taarifa za maendeleo ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii yanayoendelea nchini.

Akitoa tathmini ya masuala mbalimbali ya kiuchumi, Naibu Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais anataka kuona nchi ikipiga hatua kiuchumi na kuwataka wafanyakazi kumsaidia Mheshimiwa Rais kutimiza azma hiyo.

“Fanyeni kazi kwa uadilifu na Mheshimiwa Rais anathamini Sana mchango mnaoutoa kama ubalozi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza uchumi,” amesema Dkt Biteko.

Akitoa tathmini juu ya masuala ya Nishati hususani Kuhusu masuala ya umeme, Dkt. Biteko amesema miradi yote ya kimkakati iko kwenye hatua nzuri na kutolea mfano wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kuwa litaondoa changamoto ya upungufu wa umeme na kuwezesha vituo vya kuzalisha umeme wa maji kufanya matengenezo na kuongeza pia kiwango cha gesi ili kufidia mapungufu yaliyopo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi amewataka wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kuhakikisha wanatumia vema fursa za kibiashara zilizopo nchini Uganda kwa manufaa ya nchi yetu na kuongeza ushirikiano wa kibiashara na wadau wote.

Amesema, takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2022 uwekezaji kwenye masuala ya biashara ulikuwa karibu shilingi bilioni 138 kutoka Tanzania pekee na kuwa nchi ya tatu kwa uwekezaji nchini Uganda ambapo kikao hicho kimedhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Stephen Byabato pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Uganda.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 11, 2023
Mitaala mipya: Wizara yawatoa hofu Wamiliki Shule Binafsi