Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ameziagiza timu za Afya za Mikoa (Regional Health Management Team- RHMT) zote nchini, kujitathmini hali yao ya utendajikazi na kuona kama wanatija inayokubalika kwa taifa.
 
Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na timu ya Afya ya Mkoa wa Dodoma inayoongozwa na James Kiologwe, Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakati alipofanya ziara yake ya kwanza toka ateuliwe kushika wadhifa huo.
 
Amesema kuwa kila mmoja katika timu hiyo inayo simamia afya wajifanyie tathmini dhidi ya utendaji wao huku akisema, ametumia jukwaa hilo la timu ya Dodoma lakini na waliopo katika Mikoa Mingine yote nchini nao wajitathmini huko huko. 
 
Aidha, timu za Afya za Mkoa zimetakiwa kutambua kwamba, majukumu yao ndio maduka yao wanaotakiwa kuyafanyia kazi usiku na mchana huku wakionyesha matokeo chanya ya kile wanancho kifanya kwa kutoa taarifa kwenye ngazi husika
 
“Tatizo kubwa tulilonalo ni uratibu wa kazi, jukumu moja unakuta linakuwa na uratibu usiofahamika jambo ambayo wakati mwingine hata mtekelezaji anashindwa afanye lipi na aache lipi, hili ndilo nililo ligundua ndani ya siku zangu 30 za kuwepo katika ofisi yangu mpya,”amesema Dkt. Gwajima
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Maduka Kessy amemueleza Naibu Katibu Mkuu kwamba, ushirikishwaji wa maamuzi yaliyo mengi yamekuwa yakifanywa na Wizara moja kwa moja na kukosa uratibu wa Mkoa hali inayozua mkanganyiko wa maamuzi, sambamba na  kuwakilisha kilio chake cha uhaba wa Magari ya viongozi katika mkoa huo wakiwapo Wakuu wa Wilaya.
 
Hata hivyo, Dkt. Dorothy Gwajima aliteuliwa kushika wadhifa huo wa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya OR-TAMISEMI, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Zainab Chaula aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Mtoto aliyekatwa Koromeo mkoani Njombe afariki Dunia
Mbowe atuma salamu akiwa Gerezani