Mjumbe maalum wa Rais Rwanda aliyekuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Donald Kaberuka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweza kusimamia vizuri ukuaji uchumi wa nchi ya Tanzania.
Dkt. Kaberuka amekiri kuona maendeleo yanavyokwenda kwa kasi nchini humu, na ameziasa nchi nyingine za jirani Afrika zinahitaji kuwa na uchumi bora.
Pongezi hizo zimetolewa leo wakati Rais Magufuli alipokutana na mjumbe na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na umoja wa Afrika (AU), yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Nimefurahi sana jinsi Tanzania inavyokwenda mbele, maendeleo yanakwenda kwa kasi na Rais anafahamu kabisa kwamba katika Afrika nchi zetu zinahitaji kuwa na uchumi bora, ningependa kumpongeza Rais na watanzania wote kwa kazi nzuri wanayofanya”, amesema Dkt. Kaberuka.