Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amemsimamisha kazi Mhifadhi Wanyamapori Mkuu ambaye pia ni Mkuu wa Kanda – Pori la Akiba Rukwa lililopo wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi, Emmanuel Barabara ili kupisha uchunguzi uendelee dhidi yake.
Amechukua uamuzi huo kufuatia taarifa za raia wema kuwa, Barabara amekuwa akishirikiana na majangili katika kuhujumu rasilimali za misitu nchini.
Aidha, Kigwangalla ameagiza iundwe Kamati ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo, na endapo mtuhumiwa huyo atakutwa na hatia, hatua kali za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Utumishi wa Umma ili iwe fundisho kwa wengine.