Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla amepiga marufuku operesheni ya kukamata mifugo katika pori tengefu la Loliondo na kuagiza mifugo iliyokamatwa kuachiwa mara moja.

Amesema kuwa mifugo mbalimbali ambayo imekamatwa na bado haijafikishwa mahakamani iachiwe bila masharti yoyote na wafugaji waendelea kutumia vyanzo vya maji ndani ya pori hilo.

Aidha, Kigwangallah amesema kuwa maamuzi hayo aliyofanya ni hatua ambayo inalenga kutoa nafasi ya kushughulikia mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo ili kuleta suluhisho la kudumu.

Hata hivyo, Oktoba 19, 2017, Kigwangalla alitoa agizo kuwa mifugo na matrekta ambayo ipo kwenye pori Tengefu hilo la Loliondo viwe vimeondoshwa na kusema baada ya siku 7 mifugo na mali za watu hao vingekutwa kwenye pori hilo basi Serikali ingevitaifisha.

 

 

 

 

LIVE IKULU: Rais Magufuli akiwaapisha makatibu wakuu, naibu makatibu na wakuu wa mikoa
JPM ampa shavu Dkt. Kashillilah