Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 09 Februari, 2022. amemuapisha Dkt. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Dkt. Mabula akiapa

Kiapo hicho kimefanyika mbele ya Makamu wa Arais Dkt. Philip Isdory Mpango, Waziri mkuu Kasiim Majaliwa, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, na Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhwan Kikwete.

Rais Samia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Nchi baada ya uapisho wa Dkt. Mabula.
Rais Samia akiteta jambo na Dkt. Mabula baaya ya uapisho.

Dkt. Mabula ameapishwa leo baada ya kutokuwepo katika uapisho rasmi uliofanyika kwa pamoja ulioshirikisha mawaziri wote ambapo yeye alikuwa nje ya nchi kikazi.

Milionea aliyeendesha gari kwa kasi zaidi ashtakiwa kwa makosa ya barabarani
Mtawa afungwa kwa wizi wa pesa zaidi ya Mil 90