Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vincent Mashinji amesema kuwa baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa udiwani ambao unatarajiwa kufanyika karibuni katika Kata 48 katika mikoa 18 nchini wamepewa maelekezo kutowatangaza Madiwani CHADEMA wakishinda.

Ameyasema hayo leo kupitia mtandao wake wa Twitter na kudai kuwa hiyo itakuwa ni fursa kwao wao CHADEMA kuwaonyesha na kuwafundisha ustaarabu mpya ambao wameuanzisha.

“Wasimamizi wa uchaguzi wana maagizo ya kutowatangaza madiwani wa CHADEMA watakao shinda. Hii ni fursa kwetu kuwafundisha ustaarabu mpya. Na imani maneno haya utayakumbuka nikupe mshahara, nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani kashinda,”amesema Mashinji

Aidha, mbali na hilo Mashinji amejibu hoja ya Rais ambayo aliitoa akiwa Mwanza kuwa wezi ambao walikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikimbilia CHADEMA na kudai kuwa watu hao ambao wanatoka CCM na kwenda CHADEMA wameamua kuokoka.

 

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuhama kwa wanachama kutoka Chama cha Mapinduzi CCM kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wameokoka hivyo wameenda sehemu sahihi.

Nyalandu: Kuhama CCM nimefuata ushauri wa Baba wa Taifa
Serikali kudhibiti usafiri wa majini