Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Switbert Mkama amewaasa maafisa mazingira na wakaguzi wa migodi kuwa waadilifu ili kutimiza azma ya Serikali ya kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Mkama ametoa wito huo, wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa Maafisa Mazingira na Wakaguzi wa Migodi kuhusu Mikataba ya Minamata na Basel kwa ajili ya kupunguza matumizi ya Zebaki iliyoanza Mei 3, 2023 jijini Dodoma.

Amesema, Tanzania ilisaini Mkataba wa Tanzania ilisaini Mkataba wa Minamata kuhusu zebaki Oktoba 10, 2013 kwa lengo la kupunguza matumizi ya kemikali hiyo yenye athari kwa afya na mazingira huku akiwaasa wakaguzi kuwa waadilifu katika shughuli zao kwani bila uadilifu kama nchi tutakwenda mbele hatua moja na kurudi nyuma katika kupunguza matumizi ya zebaki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Utunzaji wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usamamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Redempta Samuel amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutatua changamoto za kimazingira.

Amesema, shughuli nyingi za uchimbaji mdogo wa dhahabu zinafanyika katika maeneo ya vyanzo vya maji na misitu na kuhusisha uharibifu wa mazingira hivyo warsha itawapa uelewa kukabiliana na changamoto hizo huku Lucas Maselo kutoka Tume ya Taifa ya Madini akisema mafunzo yatawajengea uwezo wa kuanza kuchagiza matumizi ya teknolojia ya kisasa ya uchenjuaji wa dhahabu badala ya zebaki.

Maji yamezidi unga jijini Paris Ufaransa
Julio awatuliza Viongozi, Mashabiki KMC FC