Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la wahariri na wadau wa uhifadhi, mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji litakalo fanyika decemba 19, 2022 mkoani Iringa.
Akizungumzia kongamano hilo, mjumbe wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MACIRA) Manyerere Jackton, amesema kuwa maandalizi yamekamilika huku kauli mbiu ikiwa ni ‘mazingira yetu ni uhai wetu, tuyalinde, tuyatunze,tuishi”
”Makamu wa Rais kwa kuzingatia uzito wa shughuli amekubali kushiriki kongamano hili kwa kutwa nzima kwetu sisi ni heshima lakaini nasema hii ni heshima kubwa kwa wahifadhi wote wa mazingira na kwa nachi yetu ambayo kwa sasa imejitoa kinagaubaga chini ya uongozi wa Rais Samia kuhakikisha watanzania tunashiriki kwa kila hali katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi duniani”
”Iringa si mbali na hifadhi ya Ruaha, hifadhi hii kwa takribani siku 130 mto wa Ruaha mkuu hautririshi maji sasa yote haya tukae tuzungumze tuone namana gana ya kutoka kwenye huu mkwamo leo nchi yetu ipo kwenye mgao wa umeme, tupo kwenye mgao wa maji yakunywa”
”tunasema haya mambo mengine yapo ndani ya uwezo wetu na uwezo wetu ni sisi wanahabari kusukuma kuweka msukumo madhubuti ili watala, watunga sera na wananchi wakawaida kwa wingi wao waweze kujua faida za utunzaji wa mazingira”