Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameendelea na ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma, ambapo katika moja ya hotuba zake amewataka wananchi kuchukua tahadhari.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambapo amewasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Corona.
”Corona Wimbi la tatu limeshaingia katika mkoa wetu wa Kigoma. Kati ya mikoa 10 yenye wagonjwa wengi na Kigoma imo. Kabla ya tarehe 10 mwezi huu wa saba tayari tulikuwa na wagonjwa 18, na wimbi hili linaonekana kali kweli, hivyo mzingatie sana maelekezo tusije tukaangamia” – Dk. Philip Mpango, Makamu wa Rais.
Aidha amewaagiza viongozi wa serikali kuendelea kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwani mkoa wa Kigoma unatajwa kuwa kati ya mikoa kumi inayoongoza kwa maambukizi nchini.