Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde amewataka maofisa elimu wa sekondari na halmashauri nchini kwa kuhirikiana na wadau wengine wa wa watoto kuhakikisha wanasimamia usalama wa watoto wawapo shuleni na kuhakikisha jamii inawalinda watoto na kuweka mazingira yatakayo waepushana ukatili.

Ametoa rai hiyo wakati akizuungumza katika mafunzo ya kutoa muongozo wa programu ya mradi wa kuinua wa elimu ya sekondari huku akisema, “tushirikiane tuwalinde watoto hawa pale wanapoingia kwenye matatizo ikiwemo ya kiusalama kwa kunyanyaswa kijinsia, ambapo jitihada zetu na ustawi wa jamii ni muhimu kuimarisha nguvu kwa pamoja kuhakikisha tunatibu changamoto hizi zinazowapata watoto ni wajibu wetu kuhakikisha tunasimama imara.”

”Usala wa watoto wawapo nyumbani, kwenye jamii na mashuleni ni muhimu ila lazima tutambue vihatarishi vya watoto wetu kwasababu utaviona na pale ambapo kuha vihatarishi kwa watoto wetu tuchukue hatua,” alisema Dkt. Msonde.

“Unapoona mtoto anaanza kutokuja shule au utoro wa rejareja lazima tujiulize kuna kitu gani kimemsibu kama alikuwa mhudhuriaji mzuri leo anaacha kuja shule tuwaulize vizuri tuwadadisi kwa upole waweze kuwaeleza kitu gani kinachowasibu.”

Urembo uliopitiliza ni ukatili kwa watoto
Putin agoma kupoa vita ya Urusi, Ukraine