Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa kufanya vizuri katika mashindano ya CECAFA.

Amesema kuwa kwa hatua iliyofikiwa na Zanzibar Heroes ni kubwa hivyo inahitaji pongezi kwa jitihada ilizozifanya mpaka kufikia hatua ya fainali katika mashindano hayo.

“Zanzibar Heroes wanastahili pongezi kubwa sana kwa kuonyesha juhudi za dhati mpaka kufikia hatua ya fainali, niwaombe tu wasikate tamaa, wajipange tena vizuri ili waweze kufanya vizuri katika mashindano mengine,”amesema Dkt. Mwakyembe

Aidha, amesema kuwa mafanikio hayo ni ya kujivunia kwani Zanzibar Heroes ilionyesha kandanda safi lenye ushindani wa hali ya juu.

Hata hivyo, Zanzibar Heroes ilifungwa na Harambe Stars kwa penati 5-3 katika fainali iliyochezwa nchini Kenya na kuwafanya wenyeji kuibuka mabingwa wa mashindano hayo.

 

Aina tata tano za ndoa
Hijab yamponza muhitimu sheria