Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele katika Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Mwele Malecela amefariki dunia Februari 10, 2022 mjini Geneva, Uswisi wakati akipatiwa matibabu.

Dk Mwele ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kabla ya kuvuliwa wadhifa huo na Hayati Dkt John Magufuli Desemba 17, mwaka 2016.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele wa WHO, Dk Mwele alikuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Espen), wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.

Dkt Mwele amezaliwa Machi 26, 1962 aliwahi kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aluyemnyima jirani kitanda cha kulala avunjiwa nyumba.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 11, 2022