Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameagana na aliyekuwa mwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania, Shalini Bahuguna Ikulu, Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi ameagana na Kiongozi huyo hii leo Juni 6, 2023 na kumshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Zanzibar kwa kipindi cha Miaka minne alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika ustawi na Maendeleo ya watoto nchini.

Kwa upande wake Bi. Shalin naye amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano, na kumpongeza kwa utendaji wake, kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.

Katika kipindi chake cha Miaka minne, Bi Shalini amefanikisha uboreshaji wa huduma za chanjo kwa Watoto chini ya miaka mitano, utoaji wa lishe bora pamoja na kuimarisha mfumo wa huduma za dharura kwa ushirikiano na watoa huduma za afya ngazi ya jamii.

Aparelhar bodog casino Halloween Acostumado
Ujenzi Viwanja vya michezo Dar, Dom kugharimu Bil. 54