Waziri wa Mambo ya Ndani,  Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua kampeni za Chama cha mapinduzi katika uchaguzi mdogo  jimbo la Longido unaotarajiwa kufanyika January 13, 2018 na kusema kwamba wapinzani wameogopa kushiriki kwa sababu wataachwa mbali sana.

Ameyasema hayo  wakati akizindua kampeni hizo, Dkt. Nchemba  amewataka wananchi wa jimbo la Longido  kumchagua mgombea wa CCM Dkt. Steven Kiruswa awe mbunge wao kutekeleza ilani ya chama mapinduzi kwa kuwaletea maendeleo ambayo wameyakosa kwa miaka miwili.

Dkt. Mwigulu amesema wapinzani wameogopa kuwa  wataachwa mbali katika baada ya kupima uitikio wa wananchi ambao wanakubali kazi za Rais John Magufuli na serikali ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatekeleza ilani ya CCM kwa vitendo na wananchi wanaona.

Hata hivyo,  Dkt. Nchemba amewahakikishia wananchi wajitokeze siku ya kupiga kura kwani usalama ni wa uhakika wakati wa kupiga kura.

Majaliwa afuta mfuko wa CDTF, atoa agizo kali
Video: Waziri Mkuu atoboa siri hii kwa wananchi, "Mimi kama mtendaji mkuu wa Serikali..."