Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine Ndugulile ameandika ujumbe kuhusu uamuzi wa Rais John Magufuli kutengua uteuzi wake.

Kupitia mtandao wa Instagram, Dkt. Ndugulile ambaye ni mbunge wa Kigamboni amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini na kumpa nafasi. Pia, ameahidi kumpa ushirikiano mteule mpya katika nafasi hiyo, Dkt. Godwin Mollel, Mbunge wa Siha.

“Nimepokea uamuzi wa Mhe Rais kwa unyenyekevu mkubwa. Ninamshukuru sana Mhe Rais kwa imani yake kwangu na kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. Nawashukuru @umwalimu, watendaji na watumishi wote katika sekta ya Afya kwa ushirikiano walionipatia.

Mafanikio ya sekta ni makubwa san ana ni ya kujivunia. Nafarijika kuwa sehemu ya mafanikio haya. Tuendelee kuongeza bidii kufikia malengo makubwa zaidi. Namtakia kila la kheri Naibu Waziri ajaye Dkt. Mollel na nitampatia ushirikiano wote.”

Jana, Rais Magufuli alifanya mabadiliko katika Wizara hiyo, akimteua Dkt. Mollel kuchukua nafasi ya Unaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Waislamu watakiwa kuongeza ibada, kumi la mwisho

Frank Lampard ashtuka

Waislamu watakiwa kuongeza ibada, kumi la mwisho
JPM amuondoa Dkt. Ndungulile, amteua Dkt. Mollel