Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Oktoba 3, 2023 Jijini Dar es Salaam amefanya mazungumzo na Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu, ambapo wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Utamaduni na Michezo.

Mhe. Dkt. Ndumbaro amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania inaendelea kupiga hatua katika eneo la Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Sekta hizo sasa ni biashara na zinatoa ajira kwa vijana wengi, huku akisema lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na kuongeza idadi ya wazungumzaji.

Kwa upande wake Balozi Mhe. Mehmet amesema nchi yake inakusaidia kuanzisha Kituo Cha Utamaduni hapa nchini, ambapo amesema Kituo hicho kitatoa fursa kwa waturuki kujifunza kiswahili na Watanzania kujifunza Kituruki.

Ameongeza kuwa, nchi hiyo ipo tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya michezo na kwamba Klabu ya Fernabache ya nchini humo ina nia ya kuanzisha akademi ya michezo hapa nchini.

Aidha, Mhe. Mehmet amesema kupitia ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo, Timu za Tanzania zitaendelea kupewa kipaumbele kuweka Kambi za maandalizi ya michezo mbalimbali nchini humo

Watanzania waaswa kupunguza matumizi ya Pombe
Madrasat Hidaya kuongoza Ibada maalum kuliombea Taifa