Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim amewaasa wanasiasa wanaowania kushika dola kuwa watulivu na kutotumia lugha za kukashfiana na kupaka tope wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu.

Dkt. Salim ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Utamaduni na Uridhi kutoka Chuo Kikuu Cha Kiislamu Morogoro (MUM).

Alieleza kuwa demokrasia imeendelea kukua nchini Tanzania na kwamba hii inatoa nafasi kwa chama chochote kuweza kushika dola lakini wanasiasa wanapaswa kutumia njia bora zaidi katika majukwaa bila kurushiana maneno machafu.

“Utakuta viongozi wa vyama wenyewe kwa wenyewe wanarushiana maneno, huyu hafai mara siyo raisa wa nchi hii, sasa haya mambo kwenye siasa hayatakiwi. Ni lazima kila kiongozi wa chama cha siasa atambue wajibu wake katika jamii,”alisema Dkt. Salim.

Aliongeza kuwa hali halisi inaonesha maadili ya viongozi yameporomoka hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini wanapofanya uamuzi wa kumchagua kiongozi atakaewawakilisha ama atakayeshika dola.

 

 

Rais Putin Amsafisha Sepp Blatter
Simba Yajipeleka Kimataifa Kidijitali