Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, ametangaza atakuwa tayari kuoa endapo atapata mwanamke ambaye anamuhitaji.

Amesema kuwa kwa sasa hana mpango wowote wa kurudiana na wanawake ambao amezaa nao watoto nchini Tanzania bali anatafuta mwanamke mwingine mpya ambaye atamuoa.

“Nikimpata anayenihitaji na mimi nikamuhitaji nitaoa , saizi nipo tu kwanza nasubiri ila siyo kama sina mpenzi kwani wapenzi huwa hawakosekani mnakutana, mnapendana lakini mjue kuwa mpenzi na mke ni watu wawili tofauti. Siwezi kabisaa kurudiana na wazazi wenzangu kwani hicho kipindi kimepitwa na wakati saizi nataka mpya,”amesema Dkt. Shika

Hata hivyo, Mbali na hilo Dkt. Shika amesema kuwa hawezi kuhama katika nyumba ambayo anaishi kwa kuwa anaishi bure kwenye nyumba hiyo hivyo ataondoka endapo atapata nyumba yake ila kuondoka na kwenda kupanga ni jambo ambalo hataliweza na kuwa hata huyo rafiki aliyempa nyumba hiyo atamshangaa.

 

Coutinho kutimkia Barcelona
CCM yazidi kunawili, wapinzani wengine 19 wajiunga