Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbrod Slaa amejibu kile kilichowahi kuelezwa na baadhi ya watu kuwa alipewa Ubalozi kama ‘hongo’ ya kuunga mkono Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza hivi karibuni kwenye mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Dkt. Slaa alikanusha taarifa hizo akieleza kuwa alimpa masharti Rais wa wakati huo, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa asimpangie kutekeleza ilani ya chama badala ya ilani ya nchi.

“Watu wengi mpaka leo wanaamini kuwa mimi nilihongwa kuingia kwenye ubalozi kwa kupitia Chama cha Mapinduzi, lakini mimi sikuhongwa, wala sija compromise huo uamuzi wangu wa kutoshiriki siasa za vyama. Na bahati nzuri hata Rais wangu aliyeniteua nilimwambia usije ukaniambia nitekeleze ilani ya chama fulani, nilimwambia nitatekeleza ilani ya nchi ambayo inaongozwa na chama kilichoshinda,” alisema Dkt. Slaa.

Mkongwe huyo kwenye vilinge vya siasa alieleza kuwa hivi sasa amejikita katika kufanya tafiti na kusoma mambo mbalimbali kujiongezea maarifa.

Angalia mahojiano kamili hapa kupata kwa undani:

Mgodi wa Barrick wabainika kwa uchafuzi mazingira
Yericko Nyerere aishauri Simba SC 2022/23