Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa amesema inafuatilia tatizo la migogoro ya ardhi ambayo imekua ikihusisha taasisi za Jeshi na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Nchi na kusababisha maeneo hayo kutoendelezwa.
Akizungumza na Dar24 katika mahojiano maalum, Waziri wa Wizara hiyo Det. Stergomena Tax amesema Wizara inatambua uwepo wa migogoro hiyo na ni swali ambalo amekua akiulizwa mara kadhaa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano katika vikao vyake.
“Hilo swali nimeulizwa sana hata Bungeni, baadhi ya wabunge wanalalamika kuwa sehemu za majimbo yao ina migogoro kati ya Majeshi na Wananchi, ni swala ambalo nimelifuatilia na nimeshasema haitakiwi kuwa na mahusiano hayo mabaya,” amesema.
Dkt. Stegomena ameongeza kuwa kwa kutambua uwepo wa sala hilo Serikali kupitia wizara yake imeandaa mpango wa miaka 3 wa kuondoa migogoro hiyo ambao utashughulikia tatizo hilo na Julianna 2020/2021 na utaisha 2022/2023 ikiwa kwa sasa upo katikati ya utekelezaji.
“Kwa sasa wataalam wapo sehemu mbalimbali za Nchi ambazo zimeainishwa na kuna baadhi migogogoro imeshatatuliwa na kuna sehemu bado inaendelea kutafutiwa ufumbuzi,” Dkt. Stergomeana ameongeza.
Amesema Suala hili linahitaji nguvu ya pamoja kwa Kuwa kama taasisi za Jeshi pekee haziwezi kuimaliza bila kushirikiana na wananchi.
“Kuna wakati au eneo linahitajika na Jeshi, na tunawashirikisha wananchi na tunaongea nao kama wanahitaji fidia tunawalipa na tuachukua eneo lao, lakini tunawaombva kama wao wanahitaji ulinzi huu basi watoe ushirikiano, na pia kwenye maeneo yetu ambayo tunayo tunawaomba wasiyaingilie kwa sababu watakwaza kazi zeru na migogogoro haitaisha itakua ni ya kila mara,” aliongeza.
Hata hivyo Dkt. Stergomena amewashukuru wananchi ambao huwa wanakubali kujitolea maeneo yao kwa jailli ya Jeshi kupitia serikali ya Kijiji.