Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akiwa anaendelea na ziara yake nchini Indonesia, ametembelea Chuo Cha Diplomasia cha nchini humo.

Kufuatia ziara hiyo, Tanzania na Indonesia zimekubaliana kuanzisha ushirikiano baina ya Vyuo vya Kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Pia, wamekubaliana uendeshaji wa chuo na Program za mafunzo kwa Wanadiplomasia, na kubadilishama ujuzi kwa walimu na wanafunzi wa vyuo hivyo.