Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amemkingia kifua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kujibu swali kuhusu Serikali kutoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa Machi 24, 2018, ambao mbali na masuala ya kiroho, ulitaja changamoto za kijamii.
Swali kuhusu Kanisa la KKKT iliyoandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka huo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, limeulizwa bungeni katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na mbunge wa Vunjo James Mbatia (NCCR-Mageuzi).
Aidha, katika swali lake, Mbatia ametaka kujua ukweli kuhusu barua hizo lakini baada ya kumaliza kuuliza swali hilo, Dkt. Tulia amesema haliwezi kujibiwa na kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni.
“Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima,” amesema Mbatia na kuitaka Serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani.
-
JPM afanya uteuzi mwingine
-
Tuzo za Mo Dewji kuchochea ushindani Simba SC
-
Majaliwa: Hatuwezi kutangaza ongezeko la mishahara hadharani