Muda mfupi baada ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza majina ya matano yaliyochaguliwa katika mchakato wa kumpata mgombea mmoja, taharuki ya surprise ya wasiotarajiwa sana imeibua mengi.

Kwa mujibu wa ripoti za kuaminika kutoka kwa ripota aliyeko mjini humo, makundi ya vijana wameonekana kuanza kufanya maandamano huku wakilitaja jina la Edward Lowasa, aliyekuwa mmoja kati ya wagombea ambao hawakuchaguliwa.

Hata hivyo, maandamano hayo yamedhibitiwa na wana usalama ambao wametapakaa kila kona ya eneo lililo karibu na jengo la makao makuu ya chama hicho pamoja na sehemu nyingine za mji.

Katika hatua nyingine, harufu ya rushwa imenukia katika mji huo wakati ambapo vikao vya kutengua kitendawili vikiendelea ambapo mtu mmoja mwenye asili ya bara Asia amekamatwa akiwa na fedha nyingi zinazodaiwa kuwa zilipangwa kutolewa na mgombea mmoja kuwashawishi watu.

Mtu huyo ambaye jina lake halikufahamika haraka alikamatwa katika sehemu ambayo iko mbali na lilipo eneo la tukio na alikanusha kuwa fedha hizo zina uhusiano na uchaguzi wa CCM. Maafisa usalama bado wanamshikilia mtu huyo kwa ajili ya kumhoji ili kufahamu nia yake na kutoa taarifa rasmi.

Dodoma: Hiki Ndicho Walichosema Wagombea Watano Waliopitishwa
Size 8 Amuandikia Mumewe Ujumbe Mtamu Baada Ya Kupewa Zawadi