Kwa hakika, ukiwa mwana siasa inabidi uwe na moyo mkubwa wa kupokea matokeo yoyote yatakayoamriwa juu yako na kukikabili chochote kitakachojitokeza dhidi yako.

Lakini pia, inabidi ufahamu kuwa kwenye siasa hakuna urafiki wa kudumu wala uadui wa kudumu. Upepo ukibadilika adui yako atalazimika kuwa makamo wako katika nafasi utakayoishikilia au mkajikuta kwenye sahani moja skiunga mkono au kupinga kitu fulani.

Hayo ni masomo mawili ambayo wanasiasa wengi duniani wamewahi kuyakumbushia tu kwa kuwa yako dhahiri kwa kila anayeingia kwenye uwanja huo. Hiki ndicho kinachoendelea hivi sasa Tanzania, sio CCM tu bali hata upande wa pili wa Ukawa.

Baada ya mchakato, majina matano ya wagombea waliotajwa kuingia tano bora bila shaka yalikuwa miongoni mwa majina ya watu wenye furaha zaidi watano waliopo mjini Dodoma. Lakini hivi sasa furaha yao inaweza kuwa imechanganyika na mawazo ya mchujo unaoendelea.

Haya ni maneno yaliyosemwa na wagombea hao watano baada ya kuchaguliwa ama kabla yakihusisha uchaguzi huo.

John Magufuli: “Asanteni sana, nashukuru… naombeni kura zenu,” aliwaambia waandishi wa habari.

January Makamba: “Nawashukuru wote kwa pongezi zenu. Nawashukuru wote mlioonyesha imani kwangu tangu mwanzo.” Alitweet.

Bernard Membe: “Tunapomtafuta mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM tufikiri aina ya Tanzania tunayotaka kuijenga kwa manufaa ya vizazi vya leo na vijavyo.” Alitweet July 8 na kuongeza nyingine July 11 akiwa na Lowassa.  

Asha Rose Migiro: “Hongera walioingia 5bora Nashukuru walionipongeza #UmojaNiUshindi.” Alitweet baada ya matokeo kutajwa.

Amina Salum Ali: Yeye aliretweet tweet ya CCM inayotaja matokeo ikiwa na picha ya waliochaguliwa.

Membe Akanusha Kuhusika na Aliyekamatwa na Fedha Dodoma
Dodoma: Harufu Ya Rushwa Yanukia, Vijana Waandamana