Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewatoa hofu Watanzania waliofikiri mkakati wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi hautoendelea.

Ameyasema hayo Leo Aptili 16, 2021 Bungeni Jijini Dodoma wakati akifanya hitimisho la mjadala wa Ofisi ya Waziri Mkuu taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2021 katika hoja ya kuwe na mfumo mzuri utakaohakikisha makao makuu ya Nchi Dodoma yanaendelea.

“Niwahakikishie Watanzania Dodoma inaendelea vizuri” Amesema Waziri Majaliwa.’

Aidha Majaliwa amesema kuwa Serikali imeweka mfumo mzuri wa kuhakikisha Makao Makuu ya Nchi yanaendelezwa kwa kujenga na kuendelea na mipango ya maendeleo ya Jiji la Dodoma.

Ameongeza kuwa watumishi wapo Dodoma, shughuli zote za Serikali zinafanywa, ujenzi wa miundombinu mbalimbali unaendelea.

Sambamba na hayo Majaliwa amewakaribisha waekezaji kuja kuendelea kuwekeza dodoma kwa wingi zaidi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 17, 2021
Marekani na uwekezaji wa kishindo Tanzania

Comments

comments