Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji umejipanga ili kuhakikisha kikois chao kinamaliza msimu ujao 2023/24 katika nafasi tano za juu.

Katibu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson amesema msimu uliopita ulikuwa mgumu na wenye ushindani, hivyo hawahitaji kukosea hususan katika michezo ya mzunguko wa kwanza ambayo huwa migumu sana.

Amesema kwa kutambua hilo ndio maana wameboresha benchi lao la ufundi sambamba na wachezaji watakaowasajili wakiwemo wa kigeni.

“Soka la Tanzania limekua na ndio maana msimu uliopita hadi dakika za mwisho hajulikani nani anashuka kwa kuwa kila timu ilikuwa na ubora wa hali ya juu.”

Amesema kwa kutambua hilo ndiyo maana timu imeanza maandalizi mapema mkoani Iringa na Julai 25, itaenda jijini Mbeya kuendelea na maandalizi ambapo kocha atapata nafasi ya kucheza michezo ya kirafiki.

Dodoma Jiji msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tisa ikiwa na alama 37 ikiruhusu mabao 37 ya kufungwa na 26 ya kufunga.

Jeshi lampindua Rais, lasitisha huduma taasisi zote
Usajili Simba SC wamtega Kibu Denis