Mchezo wa mzunguuko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Dodoma Jiji FC dhidi ya Maafande wa Jeshi La Magereza (Tanzania Prisons) umehamishiwa mjini Iringa kwenye uwanja wa CCM Samora.

Mchezo huo utakaochezwa Jumatatu Oktoba 26, ulikua urindime kwenye uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, lakini kutokana na uwanja huo kuwa na ratiba yamatumizi mengine, uongozi wa Dododoma Jiji FC umelazimika kuchagua uwanja wa CCM Samora.

Taarifa ya uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza msimu huu 2020/21, ilitolewa baada ya ile ya uongozi wa Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Magufuli: Sikumfukuza Gambo Ukuu wa mkoa
Apasuka korodani akiwa uwanjani