Wakati Mashabiki wa Soka nchini wakisubiri kwa hamu kubwa kuanza kwa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/22, Mshambuliaji wa Dodoma Jiji FC Cleophance Mkandala wamewachimba Mkwara Mabingwa watetezi Simba SC, kuelekea mchezo wa mzunguuko huo.

Dodoma Jiji FC iliyojizolea alama tatu za mchezo wa mzunguuko wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting kwa ushindi wa bao 1-0, leo Ijumaa (Oktoba Mosi) itakua mwenyeji wa Simba SC kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Mkandala amesema kikosi chao kipo tayari kupambana na Simba SC, na wamedhamiria kuwashangaza wadau wa soka nchini ambao hawaamini kama wanaweza kuwaaibisha mabingwa hao mara nne mfululizo Tanzania Bara.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba na kikubwa ni kuona kwamba tunapata alama tatu.” amesema Mkandala.

Tayari Mkandala ana bao moja msimu huu 2021/22, baada ya kuwafunga Ruvu Shooting bao pelee na la ushindi kwa Dodoma Jiji FC.

Hukumu ya Sabaya yapigwa kalenda
Ronald Koeman akata tamaa FC Barcelona