Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, amefunguka kuwa kikosi chao kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Juni 6, mwaka huu.

Mpunga amesema: “Hali ya kambi ipo vizuri, wachezaji pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Melis Medo anaendelea kuandaa kipigo kikali kwa Namungo FC.

“Namungo FC ni timu ambayo imekuwa na wakati mzuri katika mashindano haya kwa takribani misimu miwili au mitatu, wameonesha ubora wa hali ya juu na wana wachezaji wenye viwango, kwa sababu hizo lazima tufanye maandalizi mazuri.

“Nina Imani tutafanya vizuri kwenye mchezo huo japo nafahamu hautakuwa rahisi, lakini tupo tayari kupambania alama tatu.”

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Dodoma Jiji FC inashika nafasi ya 11 ikiwa na alama 31, huku Namungo FC ni ya tano na alama zake 39, zote zimecheza mechi 28.

Thierry Manzi: Ninakuja kusaini Simba SC
Young Africans yaifanyia umafia Simba SC