Mkoa wa Dodoma umetajwa kuongoza kwa mimba na ndoa za utotoni ambapo asilimia 51 ya wasichana wenye miaka kati ya 20 -22 wameolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 mkoni humo, ukilinganisha na asilimia 37 ya kitaifa kwa mujibu wa takwimu.
Hayo yamebainishwa na Mbuge Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Tafma Touwfiq katika uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Dodoma, amesema kwa takwimu hizo maana yake ni kwamba kati ya watoto 100, watoto 51 wanaoolewa kabla ya kufikia miaka 18.
Mbunge huyo ameongeza kuwa watoto wanaozaa wakiwa na umri mdogo ni asilimia 39 akizitaja takwimu hizi kuwa zinaonyesha tunahitaji kuongeza jitihada na kuwekeza Zaidi katika mikakati yetu ya kumuwezesha na kumuendeleza mtoto wa kike.
Amesema mkoa huo umezindua kampeni ya kupambana na ndoa na mimba za utotoni na kampeni hii ni kubwa na itaendelea hadi itakapofikia malengo ya kumkomboa mtoto wa kike na kumuweka katika mazingira salama ya kumuwezesha kufikia ndoto zake.
Ili kuonesha mkakati wa kupambana na ndoa za utotoni mkoani Dodoma Mbunge huyo amesema mkakati unaotumiwa kwasasa ni ule ujalikanao kama magauni manne akiyataja magauni hayoa kuwa gaunai la kwanza ni kuhimiza mtoto wa kike kuwa ndani ya sale ya shule, gauni la pili ni nilile la kuhitimu masomo na la tatu ni gauni la harusi na lakutiza ndoto ni gauni wakati wa ujauzito mtoto wa kike akiwa ametimiza ndoto zake.
Maadhimisho hayo yanaendelea mjini Dodoma katika ngazi ya mkoa na kaulimbiu ya mwaka huu inasema; “Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto”.