Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo leo Oktoba 5, 2018 ametoa taarifa juu ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri zote nchini kwa mwaka wa fedha wa 2017/2019 ambapo zaidi ya bilioni 5 zimekusanywa.

Mchanganuo huo wa makusanyo katika Mamlaka za Serikali za mitaa umegawanyika katika maeneo Majiji, Manispaa, Halmashauri za wilaya na Miji.

Ambapo kwa upande wa majiji, jiji la Dododma limeshika nafasi ya Kwanza kati ya majiji 6 kwa ukusanyaji mkubwa wa mapato ambapo limekusanya mapato kwa asilimia 130 huku Jiji la Mbeya limeshika nafasi ya mwisho kwa ukusanyaji mbovu wa mapato ambapo limekusanya kwa asilimia 71.

Kwa upande wa Manispaa, kati ya Manispaa 20, Manispaa ya Iringa imeshika nafasi ya kwanza kwa kukusanya mapato kwa asilimia 103 ikifuatiwa na Manipsaa ya Temeke.

Huku Mji wa geita umeshika nafasi ya kwanza kwa kukusanya mapato makubwa kwa asilimia 218 ukifuatiwa na Mji wa Njombe ambao umekusanya mapato kwa asilimia 122 huku Mji wa Nanyamba ukiwa umeshika mkia kwa makusanyo ya asilimia 54.

Na upande wa Halmashauri za Wilaya, Kibaha vijijini imeibuka kidedea kwa makusanyo ya mapato kwa asilimia 165 ikifuatiwa na Halmashuri ya Mpingwe kwa makusanyo ya asilimia 162, na Halmashauri zilizofanya vibaya kwa kukusanya mapato ya chini kabisa ni pamoja na Halmashauri ya Mbinga iliyokusanya mapato yake kwa asilimia 20 tu ikifuatiwa na Songea kwa asilimia 33 na nyingine zilizofanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato ni halmashauri ya Rolya na Siha.

Hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ametoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa kufuatilia ufujaji wa mapato yanayokusanywa na kuwachukulia hatua wahusika wote waliosababisha Halmashauri hizo kukusanya kiwango cha chini cha mapato hayo.

 

Odinga ataka Katiba mpya nchini Kenya
Video: Ali Kiba aachia ‘Mwambie Sina’ akiwa na wasanii wake