Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amewataka wananchi wa jiji la Dodoma kuzingatia usafi wa mazingira kwani ni jukumu la kila mmoja,

Amesema endapo mtu atakiuka sheria ya usafi wa mazingira katika eneo lake basi hawatasita kuchukua hatua kali.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo mbalimbali ya miradi ambayo inaendelea kutekelezwa chini ya uongozi wake.

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru

Mafuru amesema swala la usafi kwa sasa limeimarika na hii ni kutokana na kuingia mikataba na kampuni 4 za kufanya usafi katika kata nane za jiji hilo.

Pamoja na hayo Mafuru amasema kuwa Makampuni  manne ambayo wameingia ikionekana kuwa usafi hauridhishi mkataba unakuwa umevunjika.

“Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na makampuni manne lakini ndani ya mkataba huo kuna kipengele cha kuvunja mkataba kama hatutaridhika na usafi wanaofanya” Amesema Mafuru.

Ameongeza kuwa wananchi wamehamasika kufanya usafi katika maeneo yao huku akibainisha kuwa kila jumamosi wamekuwa wanapita Kata moja moja ili kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa wananchi juu ya usafi wa Mazingira na kushiriki kwa vitendo katika kufanya usafi.

Mpaka sasa Halmashauri ya jiji la Dodoma imepanda miti milioni tatu maeneo mbalimbali ikiwemo kandokando ya barabara, mashuleni na maeneo mengine huku kila mwanafunzi akikabidhiwa mti wake mmoja ambao atautunza mpaka atakapohitimu elimu katika shule husika.

Daraja la Teteriv lalipuliwa kuzuia majeshi ya Russia kuingia Kyiv
Wanaume wote Ukraine kuikabili Urusi