Kutoka nchini Nigeria kijana aitwaye Ahmed aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa uwezo wa ku Rap mbele ya Wizkid afukuzwa shule kutokana na Matumizi ya bangi.
Wakati huo mwaka 2017, Ahmed akiwa na umri mdogo, msanii wizkid aliahidi kumsaidia kwa kumpatia pesa taslim kiasi cha Naira Milioni 56.1 ikiwa ni pamoja na ahadi ya kumsaini kwenye record label yake ‘Starboyrecords’.
Taarifa za hivi karibuni ni kuwa kijana huyo amefukuzwa shule kutokana na kujihusisha na matumizi ya bangi pamoja na vikundi vya kihuni, huku wengi wakidai kuwa pengine fedha alizopewa na Wizkid ndizo alizotumia kufanya mambo maovu.
Mnamo mwaka 2017, akiwa kwenye tamasha lake la ‘Home Coming’ huko mjini Lagos Nigeria, WizKid aliahidi kumsaini kijana huyo Kwenye Label yake ‘Star Boy Records’ na kumzawadia kiasi cha pesa kisichopungua Naira Milioni 10 sawa na Tsh 56.1 baada ya kufurahishwa na uwezo wake.
“Siwezi kukosa kushukuru, Wizkid alijitahidi kufanya kila alichoweza kaajili yangu, ingawa hakuwahi kunipatia Ile Milioni 56.1, lakini ukweli ni kuwa alinifanyia vitu vya thamani zaidi ya ile M56.1 aliyoahidi, alisaidia kuwalipia kodi wazazi wangu na ada ya shule, Ila ni kweli kuwa sijawahi kuzitumia pesa zake kwajili ya kuvuta bangi” – alisema Ahmed
Mpaka sasa mwanamuziki WizKid hajazungumza chochote juu ya kuenea kwa taarifa za kuharibikiwa kwa kijana Ahmed licha ya kuwa shauku ya wengi ni kusikia tamko nyota huyo atasema nini juu ya kinachoendelea kwa Ahmed.