Rapa kutoka Ngarenaro, Arusha, Dogo Janja ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makongo ameweka wazi kuwa hatavaa tena sare za shule na kuingia darasani.

Rapper huyo amesema kuwa amejitathmini na kugundua kuwa maisha yake yanafuata mkondo tofauti na shule na kwamba ‘future’ yake haiko kwenye kusoma.

“Siku zote linapokuja suala la elimu, sio kitu cha kufanya kwaajili ya kuiga na pia unatakiwa ufuate kichwa chako kinaenda vipi. Sometimes watu wanaweza wakawa wanakuforce sana ‘soma, soma’ lakini wewe mwenyewe unakuwa unaangalia future yangu mimi haipo kwenye kusoma,”Dogo Janja ameiambia Bongo5.

“Au hata nikipelekwa kusoma, siwezi nikafanya vizuri, kwahiyo ni bora ukomboe hela za watu wanaotaka kukusaidia kukupeleka shule,” anaendelea kukakaririwa.

Amesema hata kama itatokea anasoma itakuwa anasoma vitu vingine lakini sio shule kwa maana ya kuvaa sare na kuingia darasani kuhesabu vidato.

Janjaro alikuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kuacha shule na hivi karibuni ameachia video mpya ya wimbo wake ‘My Life’ ambapo amesikika akisema kuwa ‘Msomi Nicki wa Pili, mimi niliachaga Makongo’.

Lowassa atoa ahadi kuhusu Zanzibar
Jurgen Klinsmann Kuuza Jumba Lake La Kifahari