Leo Agosti 30, 2017, Msanii chini ya lebo ya Tip Top Connection, Dogo Janja ameachia audio ya wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Ngarenaro.

Audio hiyo ambayo imeachiwa dakika chache zilizopita tayari inaonesha kufanya vizuri kutoka na namba kubwa ya wapenzi watazamaji kuitembelea.

Dogo Janja akiwa mmoja kati ya vijana wadogo walioanza kujihusisha na sanaa ya muziki mgumu Hip pop, lakini pia ni moja kati ya wasanii ambaoa wameweza kudumu katika sanaa kwa kufanya kazi nzuri zinazokubalika na kila mtu.

Katika Audio mpya ya Dogo Janja amejaribu kugusa mashabiki wake kwa kuongelea baadhi ya stori zake zilizohit sana mtaani, ambapo amejibu mashabiki na kukanusha tuhuma zilizozagaa siku za nyuma kuwa anatoka na msanii wa bongo Movie, Irene Uwoya.

Ambapo katika audio hiyo kuna mstari ameimba amesema ”Usisikilize kelele za maboya wanaosema namtamani Uwoya”.

Bonyeza hapa chini kuwa wa kwanza kuisikiliza audio hiyo.

Twaweza yatoa ripoti kuhusu upungufu wa muda wa kumwona daktari
RC Makonda awatoa hofu wananchi kuhusu bomoabomoa