Shirika la reli Tanzania TRC limesaini mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 127.2 na Kampuni ya CRRC international ya nchini China kwa ajili ya ununuzi wa behewa 1430 za mizigo ya reli ya kisasa

Wakisaini mkataba huo jijini Dar esalaam Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa amesema utengenezwaji wa behewa hizo utachukua muda wa miezi 12 hadi kukamilika kwake ambapo zitakuwa na mjumuiko wa kubeba bidhaa mbalimbali ikiwemo behewa za kubeba magari, mifugo, mafuta na bidhaa mchanganyiko

Kwa upande wake Waziri wa ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa bodi wa TRC wamesema serikali imedhamiria kuhakikisha sekta ya usafirishaji wa mizigo unaleta tija na kuongeza pato la Taifa.

Aidha Mbarawa amelitaka shirika hilo kuhakikisha linasimamia ubora wa behewa hizo na mradi ukamilike kwa wakati waliokubaliana kwenye mkataba.

Behewa hizo zinatarajiwa kukamilika na kuwasili nchini mapema Februari 25 mwaka 2023 ambapo zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kuongeza tija katika mzunguko wa biashara nchini.

Manara: Tunawakumbusha waamuzi wajibu wao
Bernard Morrison aigomea Simba SC