Ili Kuongeza ushiriki wa kiuchumi kwa wanawake na mabinti nchini Tanzania, Serikali ya Canada hii leo imetangaza kutoa msaada wa dola milioni 25 zitakazotumika katika mradi wa elimu uitwao ‘Kila Binti Asome’.

Hayo yamesemwa mapema hii leo jijini Dodoma, katika sherehe za utiaji saini wa makubaliano hayo kati ya Waziri wa Canada anayehusika na Maendeleo ya Kimataifa na Waziri wa Elimu wa Tanzania Prof. Adolf Mkenda.

Mradi huu una lengo la kuwawezesha kielimu watoto wa kike katika ngazi ya shule za msingi na sekondari Tanzania Bara na Zanzibar, na upo katika hatua za mwisho za kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ikiwemo kuwa na miaka 10 ya elimu ya lazima badala ya miaka 7.

Katika kipindi cha miaka 14, Canada imetoa zaidi ya dola milioni 250 za Canada kwenye mifumo ya elimu ikiwemo kuboresha viwango vya elimu na upatikanaji wa elimu na mradi huo utakuwa chini ya UNICEF.

Wananchi wahoji uwingi wa Majeshi nchini
Mikel Arteta afichua siri ya usajili Arsenal