Mgombea anaeongoza kwenye kura za maoni za urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump amezua gumzo baada ya kueleza kuwa Waislamu wanapaswa kuzuiwa kuingia nchini humo kwa muda.

Trump ambaye matamshi yake huwaacha watu midomo wazi mara kadhaa, ameeleza kuwa utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonesha kuwa waislamu wengi wamepandikizwa chuki juu ya Marekani.

Aliongeza kuwa wamarekani wanapaswa kulindwa hivi sasa hadi pale uongozi wa nchi hiyo utakapobaini sababu za kuwepo chuki hiyo.

Hata hivyo, Ikulu ya Marekeni imesema kuwa tamko la Trump ni kinyume na maadili ya taifa hilo na kinyume na maslahi ya usalama wa taifa.

Van Gaal Atoa Nasaha Nzito Kwa Wachezaji Wa United
Lionel Messi Auenzi Msaada Wa Ronaldinho