Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump amefyatuka tena akimshambulia mpinzani wake wa chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton akidai ni ‘shetani’.

Trump ametumia lugha hiyo chafu dhidi ya Clinton, alipokuwa akizungumza katika shule moja Pennsylvania, ambapo alimshambulia mwanasiasa mkongwe Bernie Sanders anayefanya kazi ya kumnadi Bi. Hillary Clinton, akisema kuwa anafanya kazi na shetani.

“[Bernie Sanders] anafanya kazi na shetani. [Hillary Clinton] ni shetani,” alisema Trump.

Viongozi wa Democratic wamelaani vikali matamko ya Trump hususan kuhusu namna alivyowashambulia wazazi wa mwanajeshi wa Marekani ambaye ni muislamu, Captain Humayun Khan aliyeuawa katika shambulio la bumu nchini Iraq.

Trump alizua utata baada ya kueleza kuwa wazazi wa mwanajeshi hiyo walipaswa kuzuiwa kuzungumza lolote katika mkutano wa Democratic uliofanyika wiki iliyopita kumpitisha Bi. Clinton kuwa mgombea urais.

Trump amekuwa akipingwa hata na baadhi ya viongozi wa Republican kutokana na kutoamini katika kile anachokifanya na kutoenenda kwa mujibu wa ilani ya chama hicho.

Liverpool Yaangukia Pua, Yapigwa 2-1
Bilionea Sabodo aitosa Chadema, atangaza kuwekeza trilioni 11 Dodoma