Mgombea wa nafasi ya kupeperusha bendera katika kinyang’anyiro cha Urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump ametoa kauli ya kipekee akieleza atakachofanya endapo hatachaguliwa kuwa Rais.

Akiongea Jumapili hii katika mahojiano maalum, Trump aliwaambia wamarekani kuwa wasitegemee kumuona tena endapo atashindwa.

Alisema kuwa imejengeka tabia kuwa yule anayeshindwa hujitokeza hadharani na kumpongeza aliyeshinda huku akimsifia lakini hilo halitatokea kwake.

“Wanapambana kama nini kwa kipindi cha miezi sita, na wanashambuliana kwa mambo mabaya, halafu mmoja anashidwa na mwingine kati yao anashinda. Yule aliyeshindwa anasema ‘Nataka kumpongeza mpinzani wangu. Ana uwezo mkubwa, atakuwa Gavana Mzuri au Rais mzuri or vyovyote,” alisema Trump.

“Sina uhakika kama mtakuja kuniona nikifanya hivyo. Sidhani kama nitashindwa, lakini ikitokea nimeshindwa, sidhani kama mtaniona tena. Nitaenda kucheza golf au kufanya kitu kingine,” aliongeza.

 

Petr Cech: Itakua Miujiza Kumaliza Juu Ya Spurs
2016 Ni Mwaka Wa Riyad Mahrez