Zikiwa zimepita siku mbili baada ya Fahmi Dovutwa, kuvuliwa uenyekiti wa chama cha UPDP ameibuka na kupinga uamuzi huo huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujiandaa na uchaguzi.
Dovutwa amesema hajavuliwa Uenyekiti wa chama na wanaotangaza hivyo wana hofu ya uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Desemba.
Hata hivyo, katibu mkuu wa UPDP, Hamad Ibrahim amepinga na kusema chama hicho kimemwandikia barua, Fahmi Dovutwa kumvua Uenyekiti na uanachama.
Aliyegushi ‘CV’ kupata kazi atupwa jela
Ikumbumbukwe kuwa Desemba 2, 2019 Makamu mwenyekiti wa chama hicho alitangaza Dovutwa kuvuliwa uenyekiti kwa madai ya kutangaza kuwa UPDP haitashiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24 bila idhini ya chama.