Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa amesema uwepo wa ajira za Watanzania hususan watumishi wa bandari ya Dar es Salaam ni kipaumbele kikubwa cha Serikali sio tu katika azimio hilo bali katika kila
aina ya uwekezaji ambao nchi itaufanya ambapo ibara ya 13 ya Mkataba huo inaitaka DP World kuendeleza ajira za Watumishi wote waliopo.
Mbarawa ameyaema hayo wakati akiwasilisha Bungeni maelezo ya awali kuhusu mapendekezo ya kuridhia mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari nchini.
Amesema, “kuwaajiri Watanzania pamoja kuwaendeleza kitaaluma. Vilevile,
Mkataba huu umeweka bayana sharti kwa Kampuni ya DP World kutumia Wakandarasi wa ndani katika manunuzi ya huduma na bidhaa pamoja na kusaidia Vyuo vya mafunzo vya Tanzania katika masuala
ya elimu ya usafirishaji majini.”
Aidha, ameongeza kuwa, Baadhi ya manufaa yatakayopatikana ni pamoja na kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24, hali itakayopunguza gharama za utumiaji
wa Bandari matokeo ambayo yataongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 mpaka kufikia meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33.