Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, amesema yeyote mwenye mwenye lengo la kuvuruga amani ya nchi atashughulikiwa bila kujali cheo, jinsia wala dini katika kipindi cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.

Amesema hayo wakati akizindua Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wiliya ya Mufindi, mjini Mafinga, ambapo amesisitiza kuwa jukumu la kulinda amani ya nchi ni jukumu la kila mtanzania.

”Ni vizuri kulinda amani tuliyonayo kwasababu machafuko yakitokea tutaenda wapi? nchi nyingi zinataka tuharibikiwe kwasababu wao wameshaharibikiwa hivyo ni vyema taratibu na sheria za nchi tulizojiwekea tuzifuate” amesema DPP Biswalo

Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Wiliamu amewataka wananchi kuitumia ofisi hiyo kupata haki na kulinda amani ya eneo hilo kwa maendeleo ya Taifa.

NEC yatoa ufafanuzi Lissu kuzuiwa kufanya kampeni
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 24, 2020