Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini DP,P Biswalo Mganga amewafutia mashtaka washtakiwa 57 wa Gereza la Kayanga wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera ambapo kati yao wanaume ni 54 na wanawake ni 3.

DPP ametoa msamaha huo baada ya yeye, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Godfrey Mheluka kutembelea na kukagua hali ya gereza hilo.

Aidha washtakiwa hao wamefutiwa mashtaka mbalimbali yaliyokuwa yanawakabili yakiwemo wizi wa mifugo, ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi na ugomvi wa mipaka ya mashamba.

DPP Mganga amewataka washtakiwa hao waliofutiwa mashtaka kujirekebisha na kwenda kuwa raia wema watakaporudi uraiani ikiwa ni pamoja na kujishugulisha na shughuli za uzalishaji.

Katika kundi la washtakiwa walioachiwa huru wapo raia kutoka nchi jirani ya Burundi, ambao DPP amewataka kufuata taratibu za kisheria endapo wanataka kuishi nchini.

Marekani kufadhili tena WHO
Tanzia: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma afariki dunia