Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umebeza nguvu ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dr. John Magufuli dhidi ya umoja huo utakaomsimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa ambaye taarifa za awali zinaeleza kuwa ndiye aliyechaguliwa kupeperusha bendera ya Ukawa alisema Dr. Magufuli hawezi kuwashinda kwa kuwa hata kwenye jimbo lake la Chato wamempita mbali.

Dr. Slaa alieleza kuwa kama upinzani umeweza kumpita kwa nguvu katika jimbo lake kwa kuchukua viti vingi zaidi katika ngazi za serikali za mitaa, vitongoji na udiwani hataweza kushindana nao katika nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi chini.

Ukawa wanatarajia kumtangaza rasmi mgombea wako kesho, Julai 14.

Majambazi Wavamia Kituo Cha Polisi Ukonga Na Kufanya Mauaji
Lulu Aielezea Post Yake Tata Kuhusu Urembo Na ‘Viti Maalum’