Rap Drake ameripotiwa kutia saini mkataba mpya wa dili nono na Universal Music Group ambao inasemekana una thamani ya dola milioni 400 sawa na zaidi ya Tsh Bilioni 928 .

Habari hiyo imethibitishwa kupitia simu ya mapato ya UMG (Q1 earnings call), licha ya kuwa kiasi halisi hakikuwekwa wazi lakini wadadisi wa mambo wametaja kuwa kinaweza kuwa kikubwa zaidi dola milioni 400.

Hapo awali Drake aliwahi kusaini dili na Cash Money kupitia ‘Republic Records, inazomilikiwa na Universal Music Group, na amesaini tena na UMG mkataba mpya, ambao makubaliano yatahusisha kurekodi, kusambaza kazi za muziki, bidhaa za mavazi pamoja na miradi mingine,(Recordings, publishing, merchandise, and “visual media projects).

Kwa mujibu wa wakili mmoja katika tasnia ya muziki nchini Marekani, “Drake ana uwezo wa kujadiliana ili kufikia muafaka wa mgawanyiko wa faida kamili pamoja na masharti kwa ubora zaidi Ingawa uhusiano wake na Young Money/Cash Money ambayo pia iko chini ya Universal Music Group bado unabaki kizungumkuti.

Kizungumkuti hicho kinaonekana ni kuwa pengine rapa huyo tayari amekamilisha majukumu yake yote katika mkataba wake wa awali wa UMG hata kiasi cha kufikia hatua ya kuingia makubaliano mapya huku kitita cha pesa kikiwekwa mezani kwa Drake.

Kwa mujibu wa Complex ambao waliwahi kufanya mawasiliano na wawakilishi wa Drake ili kufahamu undani wa mambo kadhaa kuhusu mikakati ya Drizzy.

Mtendaji wa rekodi na mjasiriamali Steve Stoute alisema mnamo Julai 2020 kwamba Drake alipaswa kupata siku kubwa ya malipo mara tu mkataba wake wa UMG utakapokamilika. “Drake anakaribia kupata begi kubwa zaidi katika historia ya biashara ya muziki,” alisema Stoute.

Drizzy Drake anaendelea kubaki kuwa mmoja wa wasanii maarufu zaidi duniani, ambaye mara kadhaa amekuwa akiongoza katika chati mbali mbali katika kila moja ya kazi zake za sanaa., mwezi uliopita ripoti za bilboard ziliweka wazi kwamba kupitia digital platfoms mnamo 2021 rapa huyo alizalisha streams nyingi kuliko msanii na muziki wowote kabla ya mwaka 1980 kwa US.

Usitamani kuwa maarufu, tamani kuwa tajiri:Cardi B
Rais Samia aishukuru Azam Media kwa kudhamini Ligi Kuu