Mashabiki wa Drake waliofurika kwenye onesho la rapa huyo jijini Boston, Marekani walipatwa na mshangao baada ya kumuona aliyekuwa hasimu wake, Meek Mill jukwaani.
Drake aliwashangaza mashabiki hao baada ya kumuibua Meek Mill bila wao kutarajia, na kuandika historia nyingine ya kufanya kazi pamoja tangu mwaka 2015.
Meek alipokewa na shangwe za mashabiki hao na aliwabariki kwa kuimba ngoma yake ya ‘Dreams & Nightmares’ akiwa na Drake.
Wakati shangwe zikifunika muda wote, Drake alimaliza kwa kuwapa ujumbe mashabiki hao kuwa dunia inahitaji amani na upendo zaidi na kwamba hicho ndicho wanachokifanya.
Walikamilisha muda huo jukwaani wakikumbatiana kama ishara ya upendo na amani.
“Tunahitaji amani zaidi duniani. Tunahitaji upendo zaidi duniani. Meek Mill, huyu ni ndugu yangu. Huyu jamaa ni ndugu yangu tangu siku ya kwanza. Kwahiyo, tumeweza kufanya hili mbele yenu na ni heshima kubwa kwangu kuwa mmekuwepo kushuhudia,” alisema. Drake.
Drake na Meek hawakuishia hapo, waliweka kwenye Instagram picha za tukio hilo na kueleza kuwa tukio hilo limewafanya wawe na amani zaidi na kuendelea kushirikiana kama zamani.
Taharuki ya uhasimu wa kurushiana maneno, uliosababisha kutengenezeana nyimbo za kushambuliana (diss track) ulidumu kwa takribani mwaka mmoja.
Hata hivyo, wingu la amani kati yao lilianza kutanda wakati Meek akiwa jela, ambapo Drake alipokuwa anatumbuiza jijini Melbourne, Australia alipaza sauti akiungana na kampeni ya kutaka Meek aachiwe huru, “free Meek.”
Msanii aomba aendelee kufungwa kwa kujaribu kumuua Rais Kagame
Baada ya kutoka jela, Meek alifanya mahojiano na Angie Martinez na alisema kuwa hana chuki na Drake na kwamba anaamini kuwa rapa huyo pia hana tatizo naye.
Mkali huyo kutoka MMG alisema kuwa anaweza kushirikiana na rapa huyo wa Young Money katika siku za usoni.