Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, ametoa msamaha kwa watu 26 waliokuwa wamefungwa jela kwa kupanga njama ya mauaji ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Kabila mwaka 2001.

Watu hao walihukumiwa vifo na kwa mujibu wa Mamlaka, baadhi yao wamefariki wakiwa gerezani, lakini hakuna hata mmoja ambaye amenyongwa.

Rais Laurent Kabila aliuwawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake katika kasri lake mwezi Januari mwaka 2001.

Hayati Laurent Desire Kabila – Rais wa tatu wa DRC (1997-2001)

Mara tu baada ya kumuua Rais Kabila, mlinzi huyo naye aliuwawa kwa kupigwa risasi.

Mtoto wa Laurent, Joseph Kabila mara kadhaa alikataa wito wa kuwasamehe watu hao waliofungwa kwa kumuua babake.

Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar ala kiapo
Bunge la seneti Marekani laishinda turufu ya Trump